Ijumaa, 13 Machi 2015
AJARI NYINGINE TENA :BASI LA ARUSHA EXPRESS LAPATA AJALI MBAYA YA KUGONGANA NA LORI
Ajali Arusha: Imetokea ajali ikilihusisha basi la Arusha Express Lenye namba za usajili T 206 BEF na
Lori baada ya dereva wa basi kujaribu ku-overtake na kukutana na lori
mbele yake
Jumatano, 11 Machi 2015
TUKIO KATIKA PICHA NA TAARIFA YA AWALI KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA IRINGA KUTOKANA NA AJALI YA BASI LA ABIRIA NA LORI ILIYOTOKEA MAPEMA LEO .
Mashuhuda wa ajali hiyo wakijaribu kuokoa mizigo
kikosi cha uokoaji wakiwa katika harakati za kulitoa kontena juu ya basi na kutoa miili ya marehemu
Winchi zikilitoa kontena juu ya basi
Muonekano wa basi hilo Baada ya kulitoa kontena juu
Taarifa za awali kutoka jeshi la polisi mkoani Iringa zinaeleza kuwa basi la kampuni Majinja lenye usajili wa namba T438 CDE lililolaliwa na Lori lilikuwa limebeba jumla ya watu 49, idadi hiyo ni pamoja na dereva na kondakta wa basi hilo.wengi wa watu hao wamefariki dunia idadi ya majeruhi haijajulikana bado.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa kwenye mizigo mingi ya abiria waliokuwa kwenye basi hilo kumepatikana madaftari mengi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam hivyo jeshi hilo linaendelea kufanya mawasoliano ma wamiliki wa gari hilo ili kujua kama lilikuwa limekodishwa kubeba wanafunzi wa chuo hicho ama ni mchanganyiko wa kawaida wa abiria.
Ajali imetokea changalawe Mafinga
Breaking News: kwa Taarifa tulizopokea muda huu na ambazo
hazijathibitishwa kuwa Basi la Majinja Limepata ajali eneo la Mafinga
likitokea Mbeya na inahofiwa watu wengi kupoteza maisha. chanzo mpaka
sasa inasemekana ni Lori lilikuwa linakwepa mashimo ,na ndipo
likagongana uso kwa uso na Basi hilo Taarifa kamili na Tukio katika
Picha zitafuata mara baada ya kupata uhakika kamili endelea kufuatilia
hapa, Tayari Kikosi kazi cha Blogs ya rungwe yetu kipo eneo la tukio.
![]() | ||
| Hawa ni Baadhi ya Merehemu waliokwama katika basi wanaohofiwa kufa katika ajali hiyo |
Jumanne, 10 Machi 2015
Jumatatu, 9 Machi 2015
Hatari Mtoto mwingine Albino akatwa mkono
Watoto Albino wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya kikatili na kuuawa Tanzania
Matukio ya ukatili dhidi ya albino
yanaendelea kuwa tishio nchini Tanzania baada ya mtoto wa miaka sita
kukatwa kiganja cha mkono
Shambulio hilop jipya limetokea mkoani Rukwa kusini magharibi mwa nchi hiyo.Mtoto huyo kiume Baraka Cosmas alikuwa amelala na mama yake mzazi wakati wahalifu hao walipovamia nyumba yao.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa Jackob Mwaruanda amesema kwa sasa mtoto huyo anapata matibabu hospitali na hali yake inaendelea vizuri.
Polisi inaendelea na uchunguzi kubaini wahusika.
Shambulio hilo linajitokeza wiki moja tu baada ya watuhumiwa wanne kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa mauaji ya albino, Na muda mfupi baada ya Rais Tanzania Jakaya Kikwete kukemea mauaji ya albino, ambao viungo vyao hutumika katika shughuli za kishirikina kwa imani potofu kuwa zinasaidia kuleta utajiri na madaraka.
Jumatano, 4 Machi 2015
MKUU WA MKOA WA MBEYA KANDORO AWAAPISHA WAKUU WAPYA WA WILAYA MBEYA
Wageni waalikwa waliohudhuria hafla
fupi ya kuwaapisha wakuu wa Wilaya Wapya iliyofanyika katika viwanja vya
ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mbeya jijini hapa.
Pichani ni wakuu wa Wilaya za Mkoa wa mbeya
Kiongozi wa dini ya kiislam akisomna dua katika hafla hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Zainabu Mbussi akiapa mbele ya mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Ahmad Nammohe
Mkuu wa Wilaya ya Kyela Thea Ntara
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyerembe Munasa akizungumza kwa niaba ya wenzake
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini.

Jumatatu, 2 Machi 2015
MPYAA MSANII WA BONGO MOVIE MWANADADA CHUCHU AZIRAI NDANI YA JENEZA WAKATI WA KUSHUTI MOVIE
HII ni kali ya mwaka! Staa wa sinema za Bongo, Chuchu Hans amejikuta akizirai ndani ya jeneza wakati akiigiza sini ya kifo kwenye filamu, Amani limeinyaka.
Chuchu alikumbwa na hali hiyo hivi karibuni akiwa ‘lokesheni’ ya
kuigizia filamu hiyo maeneo ya Mbezi ya Kimara jijini Dar es Salaam
ambapo sanjari na yeye, msanii mwingine aliyecheza nafasi ya mwanakwaya
naye alipoteza fahamu wakati kipande hicho kikirekodiwa.
TATIZO UHALISIA, WASIWASI
Chanzo kimoja kutoka ndani ya kundi la wasanii waliokuwa wakiigiza filamu kinasema kuwa, Chuchu alikumbwa na hali hiyo kutokana na wasiwasi na ujasiri wa kuuvaa uhusika.
Chanzo kimoja kutoka ndani ya kundi la wasanii waliokuwa wakiigiza filamu kinasema kuwa, Chuchu alikumbwa na hali hiyo kutokana na wasiwasi na ujasiri wa kuuvaa uhusika.
“Awali, Chuchu alionesha wasiwasi wa kuigiza kipande hicho cha
kumwonesha yeye yumo ndani ya jeneza akiwa amefariki dunia kwa ugonjwa
kama wa kichaa kilichotokana na msongo wa mawazo baada ya kubakwa.
“Mbaya zaidi, mwongozaji naye alisema ni lazima akiwa amelala ndani ya
jeneza awekewe pamba za kuziba matundu ya pua kama maiti wanavyowekewa,”
kilisema chanzo.
...Waombolezaji wakilia kwa uchungu.
ILIKUWA WAKATI AKIAGWA
Chanzo kikazidi kudai kwamba, taharuki yote hiyo ilitokea pale, ‘mwili’ wa Chuchu ukiagwa kwenye Kanisa la Sabato, Mbezi, Dar ambapo waombolezaji walipokuwa wakipita, binti yake, Farha (9) aliangua kilio kilichomfanya Chuchu ajikute akikata pumzi ghafla!

AMALIZA SINI, ASHINDWA KUAMKA
Ikaelezwa kwamba, ilikuwa wakati kipande hicho kimeisha huku binti yake akiendelea kulia kwa kumwona mama yake ndani ya jeneza, Chuchu hakuamka ili kuendelea na vipande vingine hali iliyowafanya watu wazima kumkagua na kugundua alizirai.

“Watu walianza kupagawa, wengine walijua ameshapoteza maisha.
Lakini Mungu mkubwa Chuchu akazinduka na kumkuta mwanaye bado akilia
kwa nguvu. Ilibidi wasanii wengine waingilie kati kumtuliza,” kilisema
chanzo.
Waombolezaji wakiwa na simanzi.
MWINGINE AITIWA MCHUNGAJI
Wakati Chuchu ‘akifufuka’, yule msanii aliyeigiza nafasi ya mwanakwaya yeye alikuwa bado chini amelala chali akiwa hajitambui kwa kile kilichokuwa kikiendelea.“Yule mwenzake ilibidi aitwe mchungaji wa kanisa hilo ambaye alikuwa jirani kwa ajili ya kumwombea japo mchungaji wa filamu hiyo alikuwa ni msanii Jimy Mafufu,” kilisema chanzo.

MASWALI ENEO LA TUKIO
Baadhi ya wasanii walianza kujiuliza nini kilisababisha hali ile kwani ilionekana kama kuna roho chafu aliyetaka kufanya mauaji ya makusudi.
Baadhi ya wasanii walianza kujiuliza nini kilisababisha hali ile kwani ilionekana kama kuna roho chafu aliyetaka kufanya mauaji ya makusudi.
“Wengine waliuliza kama kuna mtu ana vitu kama hirizi au chanjo ya mambo
ya kishirikina, ikaonekana hakuna. Lakini maswali yalikuwa mengi sana,”
kilisema chanzo.

Jeneza likiandaliwa kwa ajili ya mazishi.
CHUCHU AONGEA NA AMANI
Baada ya kuinasa taarifa hiyo, Amani lilimsaka Chuchu kwa njia ya simu yake ya mkononi na kumuuliza ambapo alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Baada ya kuinasa taarifa hiyo, Amani lilimsaka Chuchu kwa njia ya simu yake ya mkononi na kumuuliza ambapo alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Huyu hapa: “Yaani siwezi kueleza juu ya ile filamu maana ilikuwa ni
hatari tupu na sijui hata mama yangu akiiona itakuaje kwa kweli.
“Lakini kwenye ile sini yangu ndiyo ilikuwa ikihitaji hivyo, nilale kama
maiti kweli na huwezi amini lilichimbwa hadi kaburi la ukweli. Mimi
nilizimia si chini ya mara moja. Pumzi yangu ilikata hasa nilipomsikia mwanangu akilia.”
Kwa mujibu wa maswali ya kisaikolojia kwa wasanii wa maigizo, baada ya msanii kuigiza filamu inayohusu ukatili wowote, kumwaga damu, mapenzi ya kupitiliza, kifo au jambo lolote ambalo ni chungu kwa ubinadamu ni lazima aombewe na viongozi wa dini ili kuifukuza roho hiyo ya kuigizia.
Wanasaikolojia wanasema kuwa, msanii akiigiza nafasi kama hizo na
kujiacha hivihihivi kuna hatari baada ya muda kuambukizwa na uigizaji
huo ikawa ndiyo maisha yake ya kila siku. Ndiyo maana baadhi ya wasanii
wa filamu duniani kote wanaishi maisha ya sawasawa na wanavyocheza
filamu.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)