Jumamosi, 6 Septemba 2014

Mwanasheria mkuu wa Zanzibar ajitoa katika uandishi wa Katiba



Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa ni kwamba mwanasheria mkuu wa Zanzibar amemwandikia barua spika wa bunge la katiba kumtaarifu kujitoa katika timu aliyoiteua kuandika katiba baada ya vifungu kupitishwa na wabunge ambapo kwa kiasi kikubwa wamepingana na rasimu yenye maoni ya wananchi kitu kinachomfanya mwanasheria mkuu huyo kujitoa kwakuwa ni dhambi kuondoa maoni ya wenye nchi yao wananchi.
................................................. 

Dodoma. Kuna dalili hali si shwari ndani ya Bunge Maalumu la Katiba baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Othman Masoud Othman kujiuzulu ujumbe wa Kamati ya Uandishi wa Katiba inayopendekezwa.

Habari za uhakika zilizopatikana jana bungeni mjini Dodoma, zinaeleza kuwa kigogo huyo wa SMZ amemwandikia barua Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta akimwarifu juu ya uamuzi wake huo.

Kamati hiyo ndiyo moyo wa Bunge hilo katika kuandika vifungu, ibara na sura za rasimu kulingana na mapendekezo ya kila kamati na baada ya majadiliano na mwisho inawajibika kuandika Katiba itakayopendekezwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni.

Kujiengua kwake ni pigo kwa Bunge Maalumu, kwani kunapunguza uhalali wa Katiba itakayopendekezwa kwani Othman akiwa Mwanasheria Mkuu wa upande huo wa Muungano ndiye anayepaswa kuwa kinara wa kulinda masilahi ya Zanzibar wakati wa uandishi wa Katiba inayopendekezwa.

Jana Othman alilithibitishia gazeti hili kuhusu kujiuzulu kutoka kwenye kamati hiyo, lakini akakataa kueleza sababu zilizomsukuma kuchukua uamuzi huo akitaka Mwenyekiti wa Bunge Maalumu atafutwe kwani barua yake ya kujiuzulu ameikabidhi kwake.

“Ni sahihi kwamba nimejiuzulu…hizo sababu ndiyo siwezi kukutajia maana kwa mujibu wa taratibu za Bunge Maalumu zinapaswa kuzungumzwa na Mwenyekiti maana barua yangu ya kujiuzulu anayo yeye,”alisema Othman alipozungumza na gazeti hili kupitia simu yake ya mkononi jana.

Hata hivyo, Sitta alipotafutwa jana, alikataa kuzungumza lolote juu ya taarifa hizo akisema hawezi kufanya mahojiano na mwandishi asiyemfahamu kwa njia ya simu.

“Kwanza sikujui halafu unataka nifanye mahojiano kwenye simu? Mimi sipo (Dodoma), nipo Dar es Salaam ninarudi Jumatatu niliondoka huko (Dodoma) mara tu baada ya kipindi cha asubuhi,” alisema Sitta.

Kwa upande wake, Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad, alipotafutwa alisema hajaiona barua hiyo ya Othman, lakini kwa utaratibu, mjumbe anayetaka kuchukua uamuzi kama huo humwandikia barua mwenyekiti ndipo ishuke chini.

“Mimi bado sijapata taarifa hiyo, labda atakuwa amewasilisha kwa mwenyekiti akishaipata ndiyo inaletwa huku kwangu,”alisema Hamad.

Alisema kwa sababu nafasi hizo ni uteuzi unaofanywa na mwenyekiti na kanuni ziko kimya kuhusiana na idadi ya wajumbe katika kamati, mwenyekiti ndiye mwenye uamuzi wa kuteua mtu mwingine ama kuacha.


Chanzo: Mwananchi

Jumatano, 4 Juni 2014

WASANII WA RIMACO FILMS LEO WAKIENDELEA NA KITENGENEZA FILAMU MBILI, RIZIKI YANGU NA PENZI LA THAMANI

CAMERA MAN RICHARD MCHINA WAKIWA NA MUONGOZAJI ISARITO MSHINDI WA TMT (TANZANIA MOVE TALENT) NYANDA ZA JUU KUSINI.

CAMERA MAN AKIWA KAZINI

MUONGOZAJI WA FILAMU ISARITO AKIWA NA MSANII JAMES MLIMBWA

 

BAADHI YA VIPENGELE KATIKA FILAMU MUONGOZAJI ISARITO AKIMUELEZA KITU MSANII


WASANII WAKIWA KATIKA POZI BAADA YA KUMALIZA KAZI KWA SIKU YA LEO



WAKIPATA CHAKULA



PICHA NA RUNGWE YETU

Ijumaa, 30 Mei 2014

RIMACO FILM'S WANATENGEZA FILAM LEO WALIKUWA KATIKA SHULE YA SEKONDARI GOD'S BIDGE KYIMO TUKUYU.

DAVID ZINJO KUTOKA K&Z FAMILY AKIWA NA DIANA KUTOKA RIMACO FILM'S TAYARI KWA KAZI



EBANA!!!! DIANA & MARTHA KATIKA POZI BAADA YA KAZI

DIRECTOR  JAMES KULIA AKITOA MAELEKEZO KWA MWALIMU SHUPA WA PILI TOKA KULIA 


MKURUGENZI WA KAMPUNI YA RIMACO FILM'S KATIKATI AKIWA NA JAMES NA SHUPA


 DIRECTOR JAMES AKIWA ANAPATA KIDOGO BAADA YA KAZI NZITO

 DIANA AKIJIANDAA KWA AJIRI YA KUSHUTI

  
K&Z FAMILY THANK'S GOD'S BRIDGE

  MRUGENZI WA KAMPUNI YA RIMACO FILM'S RICHARD MCHINA KUSHOTO AKIWA NA DIRECTOR JAMES  KULIA PAMOJA NA MSANII MARTHA KATIKATI.

 
WASANII WAKIWA KATIKA POZI

Picha na:-  Rungwe yetu.

Jumanne, 13 Mei 2014

RWANDA YAMKATAA BAROZI MTEULE NDG. MUSSA SIWA WA TANZANIA



Rwanda imemkataa Balozi mteule wa Tanzania, Mussa Siwa, ambaye alitakia na serikali kwenda kufanya kazi kwenye ubalozi wa Tanzania nchini humo.Taarifa kutoka Rwanda na duru za ndani ya serikali ya Tanzania zimeeleza serikali ya nchi hiyo imemkataa balozi huyo kwasababu mbalimbali zikiwemo za kiusalama.

Habari kutoka ndani ya Ikulu ya Rwanda zinaeleza kuwa serikali ya nchi hiyo imemkataa balozi Siwa, baada ya kumshuku kuwa ni jasusi. Siwa kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo, alikuwa ofisa katika ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani.

Tazania kwa sasa haina balozi nchini Rwanda tangu Dr.Marwa Matiko amalize muda wake wa kufanya kazi hiyo. Nafasi hiya kwa sasa inakaimiwa na Francis Mwaipaja,ambaye kabla ya kupelekwa Rwanda alikuwa msaidizi wa katibu mkuu kiongozi, Ombeni Sefue.

Ofisa mmoja mwandamizi wa Ikulu ya Rwanda aliliambia MTANZANIA kuwa viongozi wa nchi hiyo wanachukuwa tahadhari dhidi ya wanadiplomasia wa Tanzania wanaofanya kazi nchini Rwanda , tangu nchi hizi mbili ziingie katika vita ya maneno mwaka jana.


‘’Viongozi hapa wamekuwa na hofu kubwa na Tanzania na kufanya wawe macho na watanzania wanaoishi hapa na hasa maofisa ubalozi na ndio maana wamemkataa balozi huyo mteule’’. Alisema mtoa taarifa wetu.

Wafuatiliaji wa maswala ya kidiplomasia wametafsiri kitendo hicho kuwa ni mwendelezo wa kutofautiana kati ya serikali za nchi hizi mbili.

Rwanda iliingia katika mgogoro na Tanzania baada ya kuchukizwa na ushauri uliotolewa na Raisi Jakaya Kikwete wa kuitaka serikali ya nchi hiyo kufanya mazungumzo na kundi la waasi la FDLR, ambalo limejichimbia ndani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Rais kikwete alitoa ushauri huo mbele ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin-Moon na Raisi wa Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma, wakati wa mkutano wa viongozi wa ukanda wa maziwa makuu ya afrika uliofanyika mjini Addis Abab, Ethiopia, Mei, mwaka jana.

Ushauri huo ulipokelewa vibaya na Rais Kagame na waziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi hiyo, Louise, Mushikiwabo, ambao walitoa kauli za kumdhalilisha Rais Kikwete.


Mkataba wa Vienna

Hata hivyo, Rwanda ina uhuru wa kisheria wa kumkataa balozi mteule wa kigeni kama inaona hafai kwenda kuishi nchini humo. Kifungu cha nne cha mkataba wa kimataifa wa Vienna wa mwaka 1961 unaozungumzia masuala ya kidiplomasia baina ya mataifa,kinatoa uhuru wa nchi kumkubali balozi mteule wa kigeni. Mathalani Tanzania , mwaka jana ilimkataa balozi mteule wa Ujerumani, Margit Hellwig – Boette, ambaye alitakiwa kuja kuwa balozi hapa nchini mara baada ya kumaliza muda wake nchini Kenya.

Sefue asema hana taarifa

Akizungumzia suala hilo, Sefue alisema taarifa hizo hajazipata na kwamba wizara ya mambo ya nje ndiyo inayoweza kufahamu vizuri suala hilo. ‘’Mimi sifahamu chochote kwakweli, nadhani watu wa wizara ya mambo ya nje ndiyo wanajua process (taratibu) hizi ndiyo maana hata jina la huyo balozi aliyekataliwa silijui’’ alisema.

Wizara ya mambo ya nje washangaa

Nae mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Mkumbwa Ally, alishangaa na kuhoji kuwa hizo taarifa tumezipata wapi kwani ni habari za ndani.

‘’Hizo taarifa mmezipata wapi, ni taarifa za ndani, chanzo chako cha habari ni nani’’,alihoji ally. Hata hivyo, alipoombwa kuzungumzia swali la msingi alisema suala hilo lipo nje ya uwezo wa wizara yake kwani Rais Kikwete ndiye mwenye mamlaka ya kuteuwa na kutangaza jina la mteule huyo.

“Kiujumla sijapata taarifa za uhakika kuhusu suala hilo kwa sababu uteuzi wa balozi yeyote ni ‘process’ utaratibu’’ , hivyo hatuwezi kujua jina lake mpaka uteuzi wake ukamilike ndipo tutangaziwe na mwenye mamlaka hayo ni Rais, hivyo siwezi sema chochote ‘’
alisema.

MTANZANIA lilifanya jitihada za kumtafuta Siwa bila mafanikio kuzungumzia suala hilo.

Katika siku za hivi karibuni uhusiano baina ya Tanzania na Rwanda umeonekana kusuasua na hata viongozi wa nchi hizi mbili wamekuwa wakidaiwa kukwepana katika hafla mbalimbali zinazohusu nchi zao pamoja na zile za jumuiya ya Africa mashariki(EAC).

Wiki mbili zilizopita, Rais kagame alikacha kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na zanzibar zilizofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na marais wote wanachama wa ( EAC).

Mbali na Kagame kutokuhudhuria maadhimisho hayo, pia aliukacha mkutano wa wakuu wa nchi za EAC uliofanyika jijini Arusha, lakini alikwenda nchini Kenyana kuhudhuria kikao cha viongozi wa nchi za Afrika Mashariki wanaounganishwa na mradi unaoitwa ‘ Northern Corridor Infrastructure Project’. Waziri Mkuu Pinda aliiwakilisha Tanzania katika mkutano huo.


Source: Gurudumu la Habari 

Jumanne, 1 Aprili 2014

KILICHOTOKEA KATIKA UJENZI WA MNARA WA BABELI KITATOKEA KATIKA MCHAKATO WA UUNDWAJI WA KATIBA MPYA TANZANIA

 HIKI NDO KINACHOENDELEA KATIKA BUNGE LA KATIBA


 EEE!!!!!!! MWENYEZI MUNGU MUUMBA WA MBINGU NA NCHI LIONGOZE BUNGE HILI LA KATIBA WAKAFANYE MAAMUZI YATAKAYOLETA MTENGAMANO NA MSHIKAMANO KATIKA NCHI YETU NZURI SANA YA TANZANIA AMEN!!!!!!!

HALI HII KWELI TUTAFIKAAAA?????????


Jumatano, 26 Machi 2014

ZOEZI LA KUUNDWA KWA TIMU YA TAIFA LAANZA TUKUYU


Wachezaji 29 kati ya 34 waliochaguliwa katika programu maalumu ya marekebisho ya timu ya Taifa inayoendeshwa na TFF wameshaanza mazoezi makali katika Wilaya ya Rungwe, Mbeya.


Wachezaji hao, ambao wametokea katika mikoa mabali mbali, waliingia kambini siku ya Jumamosi huku wakiongozwa na Mwalimu Salum Mayanga akisaidiwa na Patrick Mwagata, ambaye ni kocha wa makipa, Meja Joakim Mashanga ambaye ni daktari wa team na Fred Chimela ambaye ni Meneja Vifaa.


Timu ya Taifa, Taifa stars, inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager kwa mwaka wa pili mfululizo sasa, inatarajiwa kupata mabadiliko makubwa sana ndani ya miezi miwili ijayo ili ipatikane timu bora itakayoshiriki katika mechi za kufuzu kupata tiketi ya kucheza Kombe la Afrika.


Makocha wazoefu walikusanyika Lushoto takriban wiki mbili zilizopita na kufanya zoezi la kuwachagua vijana 34 ambao baadaye watachujwa na kubali 20.


Watakaochaguliwa watajiunga na Taifa Stars ya siku zote na kutengeneza timu ya wachezaji 45 ambao watahujwa tena ili ipatikane Timu ya Taifa yenye wchezaji 25.


Zoezi hili linatarajiwa pamoja na mambo mengine kuimarisha uzalendo miongoni mwa wachezaji watakaochaguliwa na hili linafanyika kwa kuhakikisha wachezaji wote wanaimba wimbo wa Taifa kila asubuhi na jioni kabla ya kuanza mazoezi.


Kila chumba cha wachezaji pia kina bendera ya Taifa, taratibu za kambi na wimbo wa Tanzania Tanzania ambavyo vinasaidia kuimarisha uzalendo miongoni mwa wachezaji.

Kocha Mayanga alisema kuwa vijana wote wako salama na wanategemea kuwapata wachezaji wazuri baada ya kambi hii.


“Tunapongeza wadhamini wetu Kilimanajro Premium Lager ambao wamefanikisha zoezi hili kwani tuna imani tutapata vipaji vikubwa mno baada ya zoezi hili na timu yetu ya taifa itakuwa bora zaidi,” alisema.


Wachezaji wamepiga kambi katika hoteli ya Landmark, mjini Tukuyu na wanafanya mazoezi katika Chuo Cha Ualimu Tukuyu.


Zoezi hili limeleta msisimko mkubwa mjini Tukuyu huku mashabiki wa mpira wakisema wana imani sasa itapatkana timu bora zaidi kwa sababu ya utaratibu uliotumika.

Ijumaa, 7 Machi 2014

WAWILI WAFARIKI DUNIA NA MAJERIHI KUMI NA TISA KATIKA AJALI MBILI TOFAUTI ZILIZOTOKEA WILAYANI RUNGWE, MOJA INAHUSISHA BASI LA SAI BABA LIKITOKEA DAR LIKIELEKEA KYELA LIMESABABISHA KIFO CHA DEREVA WA BASI HILO NA MAJERUHI KUMI NA NANE. AJALI YA PILI IMEHUSISHA BASI DOGO AINA YA DYNA MMOJA AFARIKI.

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE MHE. CHRISPIN MEELA AKIONGEA JAMBO KUSIANA AJALI HIYO





AJALI HII MBAYA IMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MIDA YA SAA NNE USIKU NI BAADA YA DEREVA KUSHINDWA KUIMUDU KONA YA MWAMBEGELE.

MASHUHUDA WAKIWA ENEO LA TUKIO.



MAREHEMU HUYU NI DEREVA WA BASI HILO ALIPOJARIBU KURUKA BILA MAFANIKIO NA BASI KUMFUATA JUU NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO,

 MWILI WA MAREHEMU UKIWA UMENASA CHINI YA BASI HILO NA KUPELEKEA KAZI NGUMU YA KUMTOA HAPO.


 MWILI WA MAREHEMU ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA 
GODRIVA MAMUYA DEREVA WA BASI HILO LA SAI BABA

 WAKIWA KATIKA JUHUDI ZA KUUTOA MWILI WA MAREHEMU

 ASKARI WAKIWA KATIKA KUHAKIKISHA USALAMA KATIKA ENEO LA TUKIO.

MWILI WA MAREHEMU UKICHOMOLEWA CHINI YA BASI.

...................................................................

AJALI YA PILI ILIYOHUSISHA BASI DOGO AINA YA DYNA T985 BPC ANEO LA KIWIRA


HILI NDIO BASI DOGO DYNA NI BAADA YA KUNYENYULIWA 


 MKUU WA WILAYA AKIWA NA MWANDISHI WETU WAKIJIANDAA KUINGIA CHUMBA CHA OPARESHEN KATIKA HOSPITAL YA WILAYA YA RUNGWE


WAKIWA NDANI YA CHUMBA WAKIMUANGALIA MEJERIHI ALIYEJERUHIWA SANA MGUU WAKE WA KULIA.


BAADHI YA MEJERUHI WAKIWA KATIKA HOSPITAL YA WILAYA YA RUNGWE

PICHA NA 

RUNGWE YETU