Jumanne, 13 Mei 2014
RWANDA YAMKATAA BAROZI MTEULE NDG. MUSSA SIWA WA TANZANIA
Rwanda imemkataa Balozi mteule wa Tanzania, Mussa Siwa, ambaye alitakia na serikali kwenda kufanya kazi kwenye ubalozi wa Tanzania nchini humo.Taarifa kutoka Rwanda na duru za ndani ya serikali ya Tanzania zimeeleza serikali ya nchi hiyo imemkataa balozi huyo kwasababu mbalimbali zikiwemo za kiusalama.
Habari kutoka ndani ya Ikulu ya Rwanda zinaeleza kuwa serikali ya nchi hiyo imemkataa balozi Siwa, baada ya kumshuku kuwa ni jasusi. Siwa kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo, alikuwa ofisa katika ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani.
Tazania kwa sasa haina balozi nchini Rwanda tangu Dr.Marwa Matiko amalize muda wake wa kufanya kazi hiyo. Nafasi hiya kwa sasa inakaimiwa na Francis Mwaipaja,ambaye kabla ya kupelekwa Rwanda alikuwa msaidizi wa katibu mkuu kiongozi, Ombeni Sefue.
Ofisa mmoja mwandamizi wa Ikulu ya Rwanda aliliambia MTANZANIA kuwa viongozi wa nchi hiyo wanachukuwa tahadhari dhidi ya wanadiplomasia wa Tanzania wanaofanya kazi nchini Rwanda , tangu nchi hizi mbili ziingie katika vita ya maneno mwaka jana.
‘’Viongozi hapa wamekuwa na hofu kubwa na Tanzania na kufanya wawe macho na watanzania wanaoishi hapa na hasa maofisa ubalozi na ndio maana wamemkataa balozi huyo mteule’’. Alisema mtoa taarifa wetu.
Wafuatiliaji wa maswala ya kidiplomasia wametafsiri kitendo hicho kuwa ni mwendelezo wa kutofautiana kati ya serikali za nchi hizi mbili.
Rwanda iliingia katika mgogoro na Tanzania baada ya kuchukizwa na ushauri uliotolewa na Raisi Jakaya Kikwete wa kuitaka serikali ya nchi hiyo kufanya mazungumzo na kundi la waasi la FDLR, ambalo limejichimbia ndani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Rais kikwete alitoa ushauri huo mbele ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin-Moon na Raisi wa Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma, wakati wa mkutano wa viongozi wa ukanda wa maziwa makuu ya afrika uliofanyika mjini Addis Abab, Ethiopia, Mei, mwaka jana.
Ushauri huo ulipokelewa vibaya na Rais Kagame na waziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi hiyo, Louise, Mushikiwabo, ambao walitoa kauli za kumdhalilisha Rais Kikwete.
Mkataba wa Vienna
Hata hivyo, Rwanda ina uhuru wa kisheria wa kumkataa balozi mteule wa kigeni kama inaona hafai kwenda kuishi nchini humo. Kifungu cha nne cha mkataba wa kimataifa wa Vienna wa mwaka 1961 unaozungumzia masuala ya kidiplomasia baina ya mataifa,kinatoa uhuru wa nchi kumkubali balozi mteule wa kigeni. Mathalani Tanzania , mwaka jana ilimkataa balozi mteule wa Ujerumani, Margit Hellwig – Boette, ambaye alitakiwa kuja kuwa balozi hapa nchini mara baada ya kumaliza muda wake nchini Kenya.
Sefue asema hana taarifa
Akizungumzia suala hilo, Sefue alisema taarifa hizo hajazipata na kwamba wizara ya mambo ya nje ndiyo inayoweza kufahamu vizuri suala hilo. ‘’Mimi sifahamu chochote kwakweli, nadhani watu wa wizara ya mambo ya nje ndiyo wanajua process (taratibu) hizi ndiyo maana hata jina la huyo balozi aliyekataliwa silijui’’ alisema.
Wizara ya mambo ya nje washangaa
Nae mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Mkumbwa Ally, alishangaa na kuhoji kuwa hizo taarifa tumezipata wapi kwani ni habari za ndani.
‘’Hizo taarifa mmezipata wapi, ni taarifa za ndani, chanzo chako cha habari ni nani’’,alihoji ally. Hata hivyo, alipoombwa kuzungumzia swali la msingi alisema suala hilo lipo nje ya uwezo wa wizara yake kwani Rais Kikwete ndiye mwenye mamlaka ya kuteuwa na kutangaza jina la mteule huyo.
“Kiujumla sijapata taarifa za uhakika kuhusu suala hilo kwa sababu uteuzi wa balozi yeyote ni ‘process’ utaratibu’’ , hivyo hatuwezi kujua jina lake mpaka uteuzi wake ukamilike ndipo tutangaziwe na mwenye mamlaka hayo ni Rais, hivyo siwezi sema chochote ‘’ alisema.
MTANZANIA lilifanya jitihada za kumtafuta Siwa bila mafanikio kuzungumzia suala hilo.
Katika siku za hivi karibuni uhusiano baina ya Tanzania na Rwanda umeonekana kusuasua na hata viongozi wa nchi hizi mbili wamekuwa wakidaiwa kukwepana katika hafla mbalimbali zinazohusu nchi zao pamoja na zile za jumuiya ya Africa mashariki(EAC).
Wiki mbili zilizopita, Rais kagame alikacha kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na zanzibar zilizofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na marais wote wanachama wa ( EAC).
Mbali na Kagame kutokuhudhuria maadhimisho hayo, pia aliukacha mkutano wa wakuu wa nchi za EAC uliofanyika jijini Arusha, lakini alikwenda nchini Kenyana kuhudhuria kikao cha viongozi wa nchi za Afrika Mashariki wanaounganishwa na mradi unaoitwa ‘ Northern Corridor Infrastructure Project’. Waziri Mkuu Pinda aliiwakilisha Tanzania katika mkutano huo.
Source: Gurudumu la Habari
Jumanne, 1 Aprili 2014
KILICHOTOKEA KATIKA UJENZI WA MNARA WA BABELI KITATOKEA KATIKA MCHAKATO WA UUNDWAJI WA KATIBA MPYA TANZANIA
HIKI NDO KINACHOENDELEA KATIKA BUNGE LA KATIBA
EEE!!!!!!! MWENYEZI MUNGU MUUMBA WA MBINGU NA NCHI LIONGOZE BUNGE HILI LA KATIBA WAKAFANYE MAAMUZI YATAKAYOLETA MTENGAMANO NA MSHIKAMANO KATIKA NCHI YETU NZURI SANA YA TANZANIA AMEN!!!!!!!
HALI HII KWELI TUTAFIKAAAA?????????
Jumatano, 26 Machi 2014
ZOEZI LA KUUNDWA KWA TIMU YA TAIFA LAANZA TUKUYU
Wachezaji 29 kati ya 34 waliochaguliwa katika programu maalumu ya marekebisho ya timu ya Taifa inayoendeshwa na TFF wameshaanza mazoezi makali katika Wilaya ya Rungwe, Mbeya.
Wachezaji hao, ambao wametokea katika mikoa mabali mbali,
waliingia kambini siku ya Jumamosi huku wakiongozwa na Mwalimu Salum Mayanga
akisaidiwa na Patrick Mwagata, ambaye ni kocha wa makipa, Meja Joakim Mashanga
ambaye ni daktari wa team na Fred Chimela ambaye ni Meneja Vifaa.
Timu ya Taifa, Taifa stars, inayodhaminiwa na Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager kwa mwaka wa pili mfululizo sasa, inatarajiwa kupata
mabadiliko makubwa sana ndani ya miezi miwili ijayo ili ipatikane timu bora
itakayoshiriki katika mechi za kufuzu kupata tiketi ya kucheza Kombe la Afrika.
Makocha wazoefu walikusanyika Lushoto takriban wiki mbili
zilizopita na kufanya zoezi la kuwachagua vijana 34 ambao baadaye watachujwa na
kubali 20.
Watakaochaguliwa watajiunga na Taifa Stars ya siku zote na
kutengeneza timu ya wachezaji 45 ambao watahujwa tena ili ipatikane Timu ya
Taifa yenye wchezaji 25.
Zoezi hili linatarajiwa pamoja na mambo mengine kuimarisha
uzalendo miongoni mwa wachezaji watakaochaguliwa na hili linafanyika kwa
kuhakikisha wachezaji wote wanaimba wimbo wa Taifa kila asubuhi na jioni kabla
ya kuanza mazoezi.
Kila chumba cha wachezaji pia kina bendera ya Taifa,
taratibu za kambi na wimbo wa Tanzania Tanzania ambavyo vinasaidia kuimarisha
uzalendo miongoni mwa wachezaji.
Kocha Mayanga alisema kuwa vijana wote wako salama na
wanategemea kuwapata wachezaji wazuri baada ya kambi hii.
“Tunapongeza wadhamini wetu Kilimanajro Premium Lager ambao
wamefanikisha zoezi hili kwani tuna imani tutapata vipaji vikubwa mno baada ya
zoezi hili na timu yetu ya taifa itakuwa bora zaidi,” alisema.
Wachezaji wamepiga kambi katika hoteli ya Landmark, mjini
Tukuyu na wanafanya mazoezi katika Chuo Cha Ualimu Tukuyu.
Zoezi hili limeleta msisimko mkubwa mjini Tukuyu huku
mashabiki wa mpira wakisema wana imani sasa itapatkana timu bora zaidi kwa
sababu ya utaratibu uliotumika.
Ijumaa, 7 Machi 2014
WAWILI WAFARIKI DUNIA NA MAJERIHI KUMI NA TISA KATIKA AJALI MBILI TOFAUTI ZILIZOTOKEA WILAYANI RUNGWE, MOJA INAHUSISHA BASI LA SAI BABA LIKITOKEA DAR LIKIELEKEA KYELA LIMESABABISHA KIFO CHA DEREVA WA BASI HILO NA MAJERUHI KUMI NA NANE. AJALI YA PILI IMEHUSISHA BASI DOGO AINA YA DYNA MMOJA AFARIKI.
| MKUU WA WILAYA YA RUNGWE MHE. CHRISPIN MEELA AKIONGEA JAMBO KUSIANA AJALI HIYO |
AJALI HII MBAYA IMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MIDA YA SAA NNE USIKU NI BAADA YA DEREVA KUSHINDWA KUIMUDU KONA YA MWAMBEGELE.
MASHUHUDA WAKIWA ENEO LA TUKIO.
MAREHEMU HUYU NI DEREVA WA BASI HILO ALIPOJARIBU KURUKA BILA MAFANIKIO NA BASI KUMFUATA JUU NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO,
MWILI WA MAREHEMU UKIWA UMENASA CHINI YA BASI HILO NA KUPELEKEA KAZI NGUMU YA KUMTOA HAPO.
MWILI WA MAREHEMU ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA
GODRIVA MAMUYA DEREVA WA BASI HILO LA SAI BABA
GODRIVA MAMUYA DEREVA WA BASI HILO LA SAI BABA
WAKIWA KATIKA JUHUDI ZA KUUTOA MWILI WA MAREHEMU
ASKARI WAKIWA KATIKA KUHAKIKISHA USALAMA KATIKA ENEO LA TUKIO.
MWILI WA MAREHEMU UKICHOMOLEWA CHINI YA BASI.
...................................................................
AJALI YA PILI ILIYOHUSISHA BASI DOGO AINA YA DYNA T985 BPC ANEO LA KIWIRA
HILI NDIO BASI DOGO DYNA NI BAADA YA KUNYENYULIWA
MKUU WA WILAYA AKIWA NA MWANDISHI WETU WAKIJIANDAA KUINGIA CHUMBA CHA OPARESHEN KATIKA HOSPITAL YA WILAYA YA RUNGWE
WAKIWA NDANI YA CHUMBA WAKIMUANGALIA MEJERIHI ALIYEJERUHIWA SANA MGUU WAKE WA KULIA.
BAADHI YA MEJERUHI WAKIWA KATIKA HOSPITAL YA WILAYA YA RUNGWE
PICHA NA
RUNGWE YETU
Alhamisi, 6 Februari 2014
MVUA KUBWA ZILIZONYESHA JIJINI MBEYA ZALETA MAFURIKO NA UHARIBIFU ENEO LA ILOLO ANGALIA PICHA
Bibi Enea mwenye umri zaidi ya miaka 80 akilia kwa uchungu kuwa vitu vyote vya ndani vimeharibika pia anamshukuru mungu kumponya na mafuriko hayo kwani alikuwa amelala maji ndiyo yamestua kitandani kwani maji yaliingia mpaka ndani |
Bibi Enea mwenye umri zaidi ya miaka 80 mkazi wa Ilolo akituonyesha jinsi maji yalivyoharibu vitu vyake
Mwenyekiti wa mataa Sinde A Anyandwile Mwansanu akiongea na waandishi wa habari
Hakika inasikitisha watoto hawa wametoka shule wanakuta nyumba yao imebomoka na mvua kubwa ilionyesha jijini Mbeya wazahi wa watoto hao hawakuwepo nyumbani
Kanisa la Moravian Ilolo likiwa limejaa maji ndani
Mama na Mtoto Wake wakiwa hawajui waanzie wapi kutoa maji yaliyojaa katika nyumba yao
Wananchi hawajui wafanyaje, wanalalamika kila mtu kwa jinsi alivyokumbwa na janga hili.
Picha na Mbeya yetu
Jumatano, 5 Februari 2014
RASIMU YA PILI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2013
RASIMU YA PILI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2013
- Published on Monday, 30 December 2013 14:40
| [ ] | 1073 Kb |
Pata Katiba
Copyright © 2014 Tume ya Mabadiliko ya Katiba. All Rights Reserved. Designed by Webdokta.
SIMULIZI ZA MZEE MANDELA
KWENYE kitabu alichoandika Mandela mwenyewe; “Long Walk To Freedom”, Mzee Madiba anasimulia safari yake ya kwanza nje ya mipaka ya Afrika Kusini.
Wakati huo alikuwa mafichoni kwa vile alikuwa kiongozi mwanaharakati wa mapambano ya ukombozi akiwa kwenye ANC.
Mwezi Desemba, 1961, ANC walipokea mwaliko rasmi kutoka Jumuiya ya PAFMECSA ambayo baadaye ikaja kuwa Jumuiya ya Nchi Huru Za Afrika, OAU.
Mwaliko ulihusu mkutano wa mwezi Februari mwaka 1962 mjini Addis Ababa, Ethiopia.
ANC ikamteua Mandela aende kuhudhuria mkutano huo. Lakini, kwa vile alikuwa anawindwa na utawala wa makaburu na polisi wake, safari ya Mandela ilibidi ifanywe kuwa siri kubwa.
ANC iliandaa mkakati wa safari ya Addis Ababa kwa umakini mkubwa. Ikaamliwa kuwa safari ya Mandela kwenda Addis Ababa ianzie Dar es Salaam.
Sasa Mandela anafikaje Dar es Salaam?
Mpango ukawa makamanda wapiganaji watatu wa ANC wakutane kwa siri na Mandela mahali pa siri pale Soweto. Wakutane hapo wakiwa na nyaraka muhimu za kumwezesha Mandela kusafiri nje ya nchi. Wapiganaji hao ni Walter Sithulu, Ahmed Kathrada na Duma Nokwe.
Wa kwanza kufika kwenye eneo la tukio na katika muda waliokubaliana alikuwa Ahmed Kathrada. Ajabu, Mandela na Kathrada wakabaini kuwa Walter Sithulu na Duma Nokwe wanazidi kuchelewa.
Mandela na Kathrada ‘machale yakawacheza’ kama tutatumia lugha ya mitaani. Haraka ukafanywa utaratibu wa Mandela kusafirishwa kwa gari hadi Bachuana Land. Na huko ilipangwa Mandela akapakizwe kwenye ndege ndogo ya kukodi. Ikafahamika baadaye, kuwa Walter na Nokwe walitegewa mtego na makachero wa utawala wa Makaburu , na hivyo, kutiwa mbaroni wakati wakielekea kwenda kukutana na Mandela pale Soweto.
Mzee Madiba anasimulia, kuwa alikuwa na hofu kuu kwenye safari ya gari kuelekea Bachuana Land, alikuwa na hofu kuwa polisi walikuwa wakifuatilia nyendo zake na kwamba wangemkamata kabla ya kuvuka mpaka kuingia Bachauana Land ( Botswana).
Mzee Madiba anasema; “Tulivuka mpaka bila matatiz na tukafika mji wa Lobatse mchana huo huo. Hapo nikaikuta simu ya maandishi kutoka Dar es Salaam ikinijulisha, kuwa safari yangu ya kwenda Dar es salaam itachelewa kwa majuma mawili.” ( Nelson Mandela, Long Walk To Freedom, pg.344-345)
Naam, majuma mawili yakatimu, na alfajiri moja, ndege ndogo ikamchukua Mandela kutoka Bachuana Land kuelekea Tanganyika. Ilitakiwa itue kwanza Mbeya.
Walipokuwa kwenye anga ya Zambia, Mandela anakumbuka kumsikia rubani akiita; “Mbeya, Mbeya, Mbeya!”
Hakukuwa na jibu kutoka Mbeya.
Na hali ya hewa ikabadilika ghafla. Rubani alikosa mawasiliano, ndege ikawa inayumba sana. Ikafika mahali, rubani ikabidi arushe ndege chini chini akifuata barabara ya gari.
Ghafla kengele ya dharura ya hatari ilisikika ndani ya ndege. Mandela akajisemea moyoni; “Huu sasa ndio mwisho wetu”
Hatimaye, tukavuka hali hiyo mbaya ya hewa. Ndege ikapaa kama kawaida. Nikaiona anga iliyo ng’avu, nikaiona milima. Maishani sijapenda kusafiri sana kwenye ndege, na safari ya ndege kutoka Bachuana Land kwenda Mbeya ni moja ya safari za kutisha kuwahi kusafiri.” Anasimulia Mzee Madiba.
Mandela anazidi kusimulia; “Pale Mbeya tukapanga chumba kwenye moja ya Hotel za mji. Tuliwaona watu weusi kwa weupe wakiwa wamekaa sehemu moja ya kupumzikia kwenye hoteli huku wakiongea kistaarabu. Kabla ya hapo sikuwahi kuwa mahali pa wazi au kwenye baa ambapo hakukuwa na sehemu maalumu kulingana na rangi za watu.
Hapo hotelini tulikuwa tunamsubiri kiongozi mmoja wa TANU, tuliambiwa kiongozi huyo angekuja kutupokea, anaitwa Mwakangale. Hatukumjua.
Kumbe! Naye alishafika muda mrefu hotelini hapo na alikuwa akitutafuta!” Anasimulia Mzee Madiba.
Naam, kiongozi huyo wa TANU ambaye Mandela hakumjua aliitwa John Mwakangale, alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya enzi hizo.
Na baada ya Mbeya, safari ya Mandela ilikuwa ni moja kwa moja kwenda Dar es Salaam. Huko Mandela akakutana kwa mara ya kwanza na Julius Nyerere, tena nyumbani kwake pale Msasani.
Nelson Mandela alipokuwa Msasani kwa Julius Nyerere alishangazwa sana na Julius. Ni yepi hayo yaliyomshangaza Nelson alipokutana na Julius
Chanzo:- Raia Mwema
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)





